エピソード

  • Matukio ndani ya UDA yanaonyesha upungufu wa sera.
    2024/08/01
    Matukio yanayoendelea ndani ya chama cha UDA ni dhihirisho tosha la umbali wa safari yetu kuwa na vyama vya kisiasa vyenye sera na msimamo. Vyetu ni vyama vinavyotumiwa tu kuwa daraja la kuingia mamlakani na baada ya uchaguzi, kudondoshwa kama kaa moto.
    続きを読む 一部表示
    5 分
  • Bunge la Kitaifa Laanza Msasa wa Mawaziri Walioteuliwa
    2024/07/31
    Bunge la Kitaifa linaanza kuwapiga msasa Mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto, katika Baraza jipya alilotangaza. Hii ni fursa adimu kwa Bunge kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba na kuonesha kuwa ni taasisi huru na inayojisimamia bila kushurutishwa na Serikali tendaji. Hii ni fursa ya Bunge kusafisha jina lake ambalo limekuwa si lolote la kujivunia.
    続きを読む 一部表示
    5 分
  • Kumbukumbu ya Hatua za Kinidhamu na Maswali ya Hatima
    2024/07/30
    Chama cha ODM kimeendelea kutoa msimamo kinzani kuhusu hatua ya viongozi wake wakuu kujumuishwa serikalini, na kuibua kumbukumbu ya hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya Wabunge wake waliotangaza msimamo wao wa kushirikiana na serikali baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita. Je, viongozi hawa wakuu wa chama hiki watachukuliwa hatua zozote. Kama sivyo, basi tusihadaiwe zaidi.
    続きを読む 一部表示
    4 分
  • Heshimu Wanahabari na Taaluma ya Uanahabari
    2024/07/25
    Maandamano yaliyofanywa na wanahabari nchini hayashinikizi lolote nje ya Katiba ya nchi. Yanashinikiza tu taaluma ya uanahabari kuheshimiwa na haki za wanahabari kulindwa kama ilivyo katika sheria za nchi. Wanahabari sio wahalifu, wao ni mwito wa kuitumikia nchi na wananchi wake.
    続きを読む 一部表示
    5 分
  • Rais Ruto Askilize Vijana Kwa Matendo, Sio Vitisho: Sepetuko
    2024/07/24
    Maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali yanamaanisha kuwa Rais William Ruto atastahili kuwasikiliza zaidi vijana wanaoandamana. Kusikiliza huku hakuwezekani katika mazingiraya kujipiga kifua na vitisho. Kusikiliza huku ni zaidi kupitia kwa matendo.
    続きを読む 一部表示
    5 分
  • Bustani ya Demokrasia
    2024/07/22
    Harakati ambayo imekuwa ikiendelezwa dhidi ya serikali lazima ikuze taifa linalosikiliza. Linalosikiliza kwa lengo la kuelewa, na kukumbuka kuwa serikali ni raia na sio vinginevyo. Government by the people, for the people...
    続きを読む 一部表示
    5 分
  • Kamwe tusiruhusu wahuni kurejea katika mitaa yetu, na siasa zetu.
    2024/07/19
    Maandamano dhidi ya serikali yameingiliwa na wahuni ambao nia yao ni kupora, kujeruhi na hata kuua na kuharibu. Jumatano wiki hii, wahuni pia wametatiza mkutano wa Azimio, wakisababisha purukushani na majeraha kwa wanahabari. Ni wakati wahuni hawa na wafadhili wao wakabiliwe vilivyo.
    続きを読む 一部表示
    4 分
  • Kuendeleza Uhuru wa Vyombo vya Habari ni Kudumisha Demokrasia ya Kenya
    2024/07/18
    Kukamatwa kwa mwanahabari mtajika Macharia Gaitho katika mazingira ya kudhalilisha na kuhujumu haki za mtu, siku moja tu baada ya mwanahabari wa Kameme kufyatuliwa risasi na polisi huko Nakuru alipokuwa akiangazia maandamano dhidi ya serikali kunaonesha kuchipuka tena kwa majaribio ya kudunisha uhuru wa vyombo vya habari unaolindwa Kikatiba. Kamwe tusikubali hilo kufanyika, uhuru wa wanahabari na vyombo vya habari ni mhimili muhimu mno wa demokrasia ya Kenya.
    続きを読む 一部表示
    5 分