『Uchumi na Biashara』のカバーアート

Uchumi na Biashara

Uchumi na Biashara

著者: Standard Media
無料で聴く

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.Standard Media アート クッキング 食品・ワイン
エピソード
  • Mbona Magari ya Umeme? | Uchumi na Biashara Podcast
    2022/12/11
    Baadhi ya kampuni za uagizaji na uuzaji wa magari nchini zimebadili mwelekeo na sasa zinajitosa katika uagizaji wa magari yanayotumia umeme. Kampuni ya hivi punde kufanya hivyo ni ya BasiGo na ya kwanza kuagiza mabasi 15 ya umeme ambayo yalitengenezwa na Kampuni ya BYD Automotive iliyo nchini Uchina. Mabasi haya tayari yamewasili nchini kupitia Bandari ya Mombasa na yanatarajiwa kutoa huduma za uchukuzi jijini Nairobi. Lakini je, mbona wafanyabiashara waanze kufuata muelekeo wa uagizaji wa magari ya umeme? Robert Menza amewahoji baadhi ya washikadau katika sekta hiyo
    続きを読む 一部表示
    15 分
  • Kuvuma kwa Utalii Krisimasi na Mwaka Mpya | Uchumi na Biashara Podcast
    2022/11/25
    Huku msimu wa Krimasi na Mwaka Mpya ukikaribia Sekta ya Utalii inategemea sana msimu huu kuimarika kutokana na watalii wa mataifa ya kigeni wanaolenga kuzuru maeneo mbalimbali ya kitalii nchini. Mojawapo ya maeneo hayo ni eneo la Pwani hususani Kaunti ya Mombasa. Je, wafanyabiashara hasa wa hoteli za kitalii wamejiandaa vipi msimu huu? Robert Menza amezungumza na Josephat Iha ambaye ni Meneja wa Mauzo katika Mkahawa wa Massai Beach.
    続きを読む 一部表示
    22 分
  • Serikali saidia, biashara zetu zazorota | Uchumi na Biashara Podcast
    2022/10/29
    Licha ya serkali kuahidi kushughulikia changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo, bado mahangaiko yanashuhudiwa mwezi mmoja baada ya Kenya Kwanza kuchukua hatamu za uongozi. Wengi wa wafanyabiashara hao wanalalamikia kuongezwa kwa bei ya mafuta, na kusababisha hasara katika sekta ya matatu. Charles Macharia, mhudumu wa teksi na Jimmy Mwangi, mhudumu wa matatu wanatishia kugura biashara hii. Mwanahabari wetu Edwin Mbugua amefanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara hao katika Kaunti ya Nyeri.
    続きを読む 一部表示
    15 分
adbl_web_anon_alc_button_suppression_t1
まだレビューはありません