エピソード

  • NenoLaBwana | Mahusiano Yenye Uhusiano Sehemu ya 1 - Mch. Paul Semba
    2023/12/17

    Somo hili lilitolewa katika mfululizo wa masomo ya siku kumi za uamsho wa kaya na familia zilizofanyika katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kiseke. Hili ni somo la kwanza katika mfululizo huo uliopewa kichwa kisemacho "Mahusiano Yenye Uhusiano" Waweza Fuatilia Ukurasa wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Kiseke: https://www.youtube.com/@kisekesdamedia --------------------------------------------- Kurasa Rasmi za Mitandao ya Kijamii za South Nyanza Conference Tufuatilie: https://linktr.ee/sncadventist --------------------------------------------- ©MawasilianoSNC2023

    続きを読む 一部表示
    58 分
  • Nyayo katika Mapambano | Pr. Paul Semba
    2023/05/15

    Katika somo hili Mchungaji Semba anatupeleka katika ajenda kuu ya sura ya tatu ya kitabu cha Mwanzo ambapo tunaona pambano kati ya Elohim na Shetani anaekuja kwa umbo la nyoka.


    Barikiwa na somo hili...

    続きを読む 一部表示
    43 分
  • Tofauti kati ya Makusudi na Maelekezo | Pr. Peter John
    2023/05/15

    Mungu analo kusudi kwa ajili ya kila mmoja wetu na kama tunakusudia kujenga familia zilizo imara ni muhimu kufahamu kusudi hilo na kuishi kuendana na hilo. Mchungaji John anatumia somo hili la pili kuelekeza juu ya umuhimu wa kufahamu makusudi haya na kuishi kulingana na maelekezo ya muumba wetu ili kujenga mahusiano imara na Mungu wetu na hatimaye wenzi wetu.


    Bwana akubariki sana.

    続きを読む 一部表示
    23 分
  • Muhuri wa Jinsia Yako | Dr. Hesperance Kilonzo
    2023/05/15

    Ungana na Dr. Hesperance katika sehemu ya pili ya mfululizo wa masomo ya afya katika mikutano ya Kihonda NET Event anapoangazia jinsi Muumbaji wetu alivyoweka mihuri ya kiungu katika jinsia zetu na namna gani tunapaswa kuishi ili kuendana na jinsia zetu hizo.

    Bwana akubariki...

    続きを読む 一部表示
    21 分
  • Nyayo za Matumaini | Pr. Paul Semba
    2023/05/15

    Sehemu kubwa tuyaonayo leo yanaweza kutupa kila sababu ya kukata tamaa na wakati mwingine kuhisi kana kwamba hakuna mahali tunaweza kupata tumaini. Mch. Semba katika somo la kwanza katika mikutano ya Kihonda NET Event anatufunulia pazia katika vita ile kubwa kati ya wema na uovu ulio chanzo cha vita, njaa, majanga na mabaya mengine mengi tunayoyaona leo. Lakini jambo jema ni kwamba vita hii itaisha na wema utashinda na hilo ndilo tumaini ambalo wakati wote tunapaswa kufuata nyayo zake...

    Barikiwa na Bwana tunapozitembelea nyayo hizi za Matumaini....

    続きを読む 一部表示
    43 分
  • Matumaini Katika Familia (I) | Pr. Peter John
    2023/05/15

    Inashangaza namna ambavyo tunafanya mambo mengi katika maisha yetu bila kuwa na ufahamu mzuri wa kile tunachokifanya. Katika somo hili Mchungaji Peter John anaturudisha katika kuifahamu thamani ya ndoa kwa kupitia kurudi kwa muanzilishi wa ndoa ambae ni Mungu muumbaji, hii yote inaanza kwa kujenga mahusiano thabiti kati ya mtu na Mungu alie muumbaji wake.

    Tunatumaini somo hili litakubariki, kwa maswali na maoni waweza kutufikia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii...

    続きを読む 一部表示
    18 分
  • Seli mbegu na Seli Yai na | Dr Hesperance Kilonzo
    2023/05/15

    Ungana na Dr. Kilonzo anapokuletea somo la kwanza katika mfululizo wa masomo 21 ya afya yatakayokuwa yakitolewa katika mikutano ya Kihonda NET Event. Katika somo hili Dr. Kilonzo anaelezea umuhimu wa kuzielewa seli hizo mbili kama msingi wa afya nzima ya mwanadamu.

    Karibu tubarikiwe pamoja na somo hili, kwa maswali, maoni na maombi usisite kutufikia kupitia kurasa zetu mbalimbali za mitandaoni.

    続きを読む 一部表示
    15 分