
Kilio cha Familia Bungoma
カートのアイテムが多すぎます
カートに追加できませんでした。
ウィッシュリストに追加できませんでした。
ほしい物リストの削除に失敗しました。
ポッドキャストのフォローに失敗しました
ポッドキャストのフォロー解除に失敗しました
-
ナレーター:
-
著者:
このコンテンツについて
Famili moja kutoka eneo la Ndengelwa kaunti ya Bungoma sasa imeitaka serikali ya Kenya na ile Canada kuingilia kati na kuwasaidia ili wakaweze kusafirisha mwili wa mpendwa wao na kumzika nyumbani kwao katika kijiji cha Ndengelwa.Elizabeth Nekesa ambaye ni mamake marehemu anadai kuwa Leonard Wandili aliyesafiri nchini Canada kikazi alifariki akiwa huko huku familia yake ikikosa kujua kiini cha kifo cha mpendwa wao .
“Niliachana na mtoto wangu tarehe mbili akiwa mzima, naomba mwili ufanyiwe upasuaji ili nielezwe mwanangu alikufa kivipi,mtoto alienda huko kikazi ,wanisaidie mwili wa mtoto wangu urudi kenya”…
Kwa sasa familia hiyo imeitaka serikali hizi mbili kuwasaidia ili wakaweze kujua kiini cha kifo cha mpendwa wao na mwili wake kusafirishwa nchini Kenya ili akaweze kuzikwa na familia yake kulingana na desturi na mila za jamii ya Bukusu.