『Unaweza Kumjibu, Lakini Je, Ni Lazima?』のカバーアート

Unaweza Kumjibu, Lakini Je, Ni Lazima?

Unaweza Kumjibu, Lakini Je, Ni Lazima?

無料で聴く

ポッドキャストの詳細を見る

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 2 Samweli 16:5–12 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya uasi wa mwanawe Absalomu.

Daudi tayari anapitia kipindi kigumu. Ameondoka kwenye kiti chake cha enzi na mwanawe mwenyewe amemwasi.

Lakini kana kwamba hayo hayatoshi, anakutana na Shimei ambaye anaanza kumtukana, kumlaumu na kumrushia mawe.

Mmoja wa watu wa Daudi anakasirika na kutaka kumuua Shimei.

Lakini Daudi anamzuia.

Daudi alikuwa na uwezo wa kujibu kwa nguvu lakini alichagua kujizuia.

Na hapa tunajifunza jambo muhimu sana:

Kuwa na uwezo wa kumjibu mtu hakumaanishi kwamba lazima umjibu.

Wakati mwingine tunapoteza muda, nguvu na amani yetu tukijaribu kujitetea mbele ya kila anayesema jambo baya kutuhusu.

Tunataka kila mtu atuelewe. Tunataka kila tuhuma ijibiwe na kila tusi lirudishwe.

Lakini si kila vita ya maneno inastahili kupiganwa.

Mithali 19:11 inatukumbusha kwamba busara humfanya mtu asiwe mwepesi wa hasira.

Na katika 1 Petro 2:23 tunamwona Yesu ambaye alipotukanwa hakurudisha matukano.

Hii haimaanishi kwamba tunapaswa kukubali dhuluma, uongo au unyanyasaji bila kuchukua hatua pale inapohitajika.

Inamaanisha kwamba hekima ni kujua wakati wa kujibu, namna ya kujibu na wakati wa kuacha jambo lipite.

Daudi hakuchukulia kila tusi kama vita ambayo lazima ashinde.

Na huenda hata sisi tunahitaji kujifunza hilo katika familia, kazini, kwenye mahusiano na hata kwenye social media.

Leo jiulize:

Je, ninajibu kwa sababu ni muhimu kusema ukweli au kwa sababu hasira yangu haitaki kunyamaza?

Kumbuka:

Si kila anayekutukana anahitaji jibu lako. Na si kila ukimya ni ishara ya kushindwa.

Wakati mwingine ushindi mkubwa ni kutokuruhusu maneno ya mwingine yaamue namna utakavyotenda.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

adbl_web_anon_alc_button_suppression_t1
まだレビューはありません