『Story Yangu』のカバーアート

Story Yangu

Story Yangu

著者: Story Yangu na Dolly Restie
無料で聴く

このコンテンツについて

Kuna story nyingi sana nyuma za watu waliofanikiwa au waliopiga hatua fulani kwenye maisha, na katika story hizo siku zote kuna somo kubwa la kujifunza.

Na ndio maana Femina Hip tumekuja na Story Yangu Podcast sehemu ambayo utapata nafasi ya kusikiliza story za watu mbalimbali, story ambazo hukuwahi kuziskia popote.Story ambazo zitakupa elimu, burudani na michongo pia. Usitamani kukosa hata episode moja

マネジメント マネジメント・リーダーシップ 出世 就職活動 経済学
エピソード
  • Story Yangu na Dolly Restie
    2024/06/11

    Hii ni story ya kusisimua ya @dollyrestie mtu aliyevunja matarajio yote ili kuunda hatima yake ya mafanikio.Akizaliwa Dodoma, Dolly aliamua kuwa njia yake ya mafanikio ipo Dar es Salaam. Alipofika Dar, kazi yake ya kwanza ilikuwa ni mhudumu wa bar (barmaid), kazi aliyofanya kwa changamoto nyingi kutokana na kuwa mwanamke. Alikumbana na wanaume wengi waliomtaka kimahusiano wakiahidi kumpa maisha bora.Dolly aliamua kuacha kazi ya uhudumu wa bar na kuingia kwenye tasnia ya ulimbwende maarufu kama Video Vixen. Alipata bahati ya kushiriki kwenye video kadhaa za wasanii wakubwa kama Barnaba, Marioo, G nako lakini umaarufu wake uliongezeka alipofanya kazi na Rayvanny. Wengi walimfananisha na Fahyma, mke wa Rayvanny.Dolly anasema ingawa kazi ya Video Vixen inadharauliwa na wengi kwa kudhani haina maadili, anaamini ni kazi itakayomfikisha kwenye mafanikio anayoyatamani. Kwa Dolly, kitu cha msingi ni nidhamu na heshima katika kazi yake.

    続きを読む 一部表示
    1 時間 9 分
まだレビューはありません