エピソード

  • Tukio la risasi Sydney:wengi wauawa akiwemo mtoto mmoja, huku wengine wakijeruhiwa.
    2025/12/15
    Polisi wametangaza shambulio la risasi nyingi huko Bondi Beach Jumapili kama shambulio la kigaidi, baada ya wanaume wawili kufyatua risasi kwa mamia ya watu waliokusanyika kwa ajili ya sherehe ya Hanukkah. Watu wasiopungua 16 wameuawa, pamoja na mtoto, katika shambulio la risasi nyingi lililosababisha vifo vingi zaidi nchini Australia tangu mauaji ya Port Arthur ya mwaka 1996. Tukio hilo limezua shutuma za kimataifa, limeongeza usalama kwenye maeneo ya Kiyahudi, limeleta hofu miongoni mwa jamii na kuzusha tena wito kutoka kwa viongozi kukemea chuki na kusimama pamoja kwa mshikamano na jamii ya Kiyahudi.
    続きを読む 一部表示
    10 分
  • Waaustralia wakabiliwa na wastani wa kusubiri miaka mitano kwa teknolojia za matibabu zinazookoa maisha
    2025/12/11
    Ripoti mpya ya kitaifa imegundua kuwa Waasutralia wanakabiliwa na wastani wa kusubiri miaka mitano kwa teknolojia za matibabu zinazookoa maisha. Ripoti inasema kuwa ingawa teknolojia za matibabu zinakua kwa kasi nje ya nchi, mfumo wa Australia bado uko polepole katika kupitisha na kufadhili teknolojia hizo mpya.
    続きを読む 一部表示
    7 分
  • Matokeo ya Cronulla 2005 yakumbukwa kwa hisia mchanganyiko
    2025/12/11
    Miaka ishirini iliyopita, maelfu walikusanyika kwenye kitongoji cha pwani cha Cronulla huko Sydney, kwa kile kilichogeuka kuwa mkutano wa vurugu dhidi ya uhamiaji kutoka Mashariki ya Kati. Leo hii, wakazi wa Cronulla na baadhi ya Waaustralia wenye asili ya Mashariki ya Kati wanasema mitazamo inabadilika. Lakini wengine wanahofia kuhusu harakati mpya zaidi zilizo na mpangilio wa kupinga uhamiaji.
    続きを読む 一部表示
    9 分
  • Wataalamu waonya kuwa msimu wa moto umeanza tunapotarajia joto kuongezeka
    2025/12/11
    Katika wiki za hivi karibuni, moto wa nyika umesababisha uharibifu wa nyumba na mali katika maeneo ya pwani ya katikati ya kaskazini ya New South Wales, Geraldton huko Magharibi mwa Australia na mashariki mwa Tasmania. Wataalamu wanaonya kuwa huu ni mwanzo tu wa msimu wa moto na nyinyi ambao mnasafiri kwa ajili ya likizo mnahitaji kuwa na ufahamu na maandalizi mkiwa mbali na nyumbani.
    続きを読む 一部表示
    8 分
  • Baraza la usalama wa chakula latoa vidokezo jinsi ya kuandaa vyakula kwa usalama ili kuepukana na magonjwa
    2025/12/11
    Kuna mambo mengi ya kushughulikia wakati huu wa mwaka, na milo yetu inaweza kuja na upande wa magonjwa. Baraza la Habari za Usalama wa Chakula la Australia limetoa vidokezo vyake bora jinsi ya kufurahia msimu kwa usalama - kwa lengo la kupunguza zaidi ya kesi milioni nne na laki tano za sumu ya chakula kila mwaka.
    続きを読む 一部表示
    6 分
  • Taarifa ya habari:serikali ya Australia yaomba msamaha rasmi kwa watu wa mataifa ya kwanza leo
    2025/12/09
    Baadhi ya habari zinazojumuisha taarifa yetu leo, *Victoria inatarajiwa kutoa msamaha kwa watu wa mataifa ya kwanza leo *Serikali ya Northern territory imepinga ziara ya umoja wa mataifa *Australia na marekani waanza mazungumzo kuhusu usalama na pia AUKUS *idadi ya vifo vinaendelea kuongezeka sudan baada ya mashambulio wiki iliyopita Kwa habari na maelezo zaidi tembelea tovuti yetu kwa sbs.com.au/swahili.
    続きを読む 一部表示
    10 分
  • Yaliyojiri Afrika:mapigano kati ya waasi wa M-23 na jeshi la DRC yaendelea
    2025/12/08
    Jason Nyakundi anatujuza kinachoendelea Afrika. Kwa maelezo zaidi elekea kwa tovuti yetu ya sbs.com.au/swahili.
    続きを読む 一部表示
    9 分
  • Wauzaji wajiandaa kwa ongezeko la wizi madukani msimu wa sherehe unapokaribia
    2025/12/08
    Kadri msimu wa ununuzi wa sherehe unapoanza, wauzaji wanajiandaa kwa ongezeko la wizi madukani. Nchini Australia kote, wizi umefikia kiwango cha juu zaidi katika miaka 21. Wataalamu wanasema kuwa ni sehemu ya mwelekeo mpana zaidi.
    続きを読む 一部表示
    5 分