『Imani Kwa Mungu Au Imani Kwa Mbinu?-Episode 2』のカバーアート

Imani Kwa Mungu Au Imani Kwa Mbinu?-Episode 2

Imani Kwa Mungu Au Imani Kwa Mbinu?-Episode 2

無料で聴く

ポッドキャストの詳細を見る

Send us Fan Mail

Katika episode hii tunachunguza namna ambavyo baadhi ya huduma na makanisa ya kizazi hiki yamehamisha watu kutoka kumtafuta Kristo kwenda kushikilia mbinu, ishara, na experiences za kiroho.

Kutoka matumizi ya mafuta, maji, udongo, vitambaa, prophetic acts, hadi “gymnastics” nyingi za kiroho , tunajiuliza: Je, hizi ni njia zinazotupeleka kwa Mungu, au zimekuwa distraction inayochukua nafasi ya ujumbe wa kweli wa Injili?

Kupitia mifano ya Yesu Kristo na mitume:

  • Yesu kutumia mate na udongo kumponya kipofu,
  • Kulisha watu 5000 kwa mikate na samaki,
  • Petro kuponya kupitia kivuli chake,
  • Paulo kupitia leso na vitambaa,

tunagundua jambo moja muhimu:

Walifanya miujiza, lakini hawakuwahi kujenga huduma zao juu ya miujiza.

Ujumbe wao ulikuwa mmoja:
Kuwaleta watu kwa Mungu.

🎙 Episode hii ni mwaliko wa kurudi kwenye Injili halisi, kumtafuta Kristo kuliko ishara, na kuhakikisha hatupendi “mkate” kuliko “Bread of Life”.

#ChristianPodcast #SwahiliPodcast #Injili #Faith #JesusChrist #ChristianLife #Truth #RelationshipWithGod

adbl_web_anon_alc_button_suppression_t1
まだレビューはありません